Sponsors

Umri wa kijana

_MY VIBE ATTRACTS MY TRIBE_

*POSITIVE EVENING VIBE*

Kuna mambo ambayo adui wako huwa anatumia kuhakikisha kwamba unaanguka katika nguzo ambayo ulikuwa umesimamia. Haswa hutazama mapungufu yako kwanza yanakuathiri namna gani katika maisha yako, mana mapungufu ni kama mlango ambao umeachwa wazi na kila mmoja anaweza kupita mara nyingi awezavyo. Hata shetani anapokuja kumwangamiza mtu ambaye anaona ni ngangari huwa kwanza havamii sehemu ambayo anajua mtu huyo  yupo vizuri atachunguza baadhi ya sehemu ambazo anajua kwamba ndipo unapoangukia mfano Wewe ni mtu wa hasira kila muda kwahiyo atahakikisha kwamba hachezei hiyo nafasi, kama wewe ni mtu wa kusema wengine atahakikisha kwamba anatumia hiyo sehemu kuharibu muunganiko wako na watu ambao ni muhimu katika maisha yako kama marafiki au hata wanafamilia wenzako, kama wewe kuna muda unakuwa  mwongo atahakikisha kwamba anatumia hilo pungufu lako katika sehemu ambayo hutaki kutumia uongo wako ili aweze kukuangamiza mfano kazini ba mwisho wa siku utafukuzwa.

Hatuwezi kuwa sawa muda wote lakini kunamapungufu ndani yetu lazima tuyajue ili tuweze kusonga mbele na kumbuka kwamba sio kila mmoja atafurahi kuona kwamba unasonga mbele haswa wale ambao wanamtumikia shetani kwa kuwa na tabia kama ambazo nimezitaja hapo juu. Kunamsemo mmoja unasema kwamba *Understanding  yourself is knowledge,understanding others is wisdom* huu msemo unamaanisha kwamba _kujielewa mwenyewe ni Maarifa na kuelewa wengine ni Hekimaa_
Hizi ni sehemu mbili ambazo adui mkubwa katika maisha yetu (shetani) anahakikisha kwamba  huvioni na usivielewe na ukikosa maarifa na Hekima jua utakosa kujiongoza. Nikwambie kitu kimoja kwamba katika maisha ukikosa kujiongoza (self control)  utaongozwa na kila mmoja mana hata akili itakuwa katika muundo wa kusubiri amri na kukubali jambo lolote mbele yako.Nini matokeo yake?? Utashundwa kuwa  na malengo thabiti, utashindwa kuwa na msimamo hata katika familia yako,utashindwa kufanikiwa katika malengo yoyote ambayo utajaribu kuweka, utashindwa kuwa na furaha wewe pamoja na familia yako n.k.
Cha msingi ni kusimama imara acha maisha ya kujipanga kabla ya kumweka Mungu mbele ndipo ujipange. Mambo yako yaweke mbele za Mungu hata kama uko wakati mgumu ili usitetereke.

_SIPENDI MWAKA HUU NIKUACHE, HEBU TWENDE PAMOJA-@2017_
Source mikazi

No comments:

Post a Comment